Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Ukaribisho

profile

DKT. DAVID J MWASOTA, DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA NDANI
Kaimu Mganga Mfawidhi

Napenda kukukaribisha katika Tovuti hii ya Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida. Katika tovuti hii utapata taarifa muhimu sana, za uhakika kuhusu huduma zetu. Mimi na watumishi wote wa hospitali hii tupo tayari kabisa kukuhudumia, hivyo karibu upate huduma zetu za matibabu ya kawaida na ya kibingwa. Kwa sasa tunahudumia wasatani wa wananchi 300- 600 kwa siku na tuna jumla ya vitanda 275 na wodi 13 na wastani wa wagonjwa wanaolazwa kwa siku ni 136. Wakati wowote tunakukaribisha na usisite kuwasiliana nasi kwa jambo lolote linalohusu huduma zetu.