Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Background

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida ilijengwa mwaka 1954 kwenye eneo la hekta 1.5 ikitumika kama Hospitali ya Wilaya. Ilipandishwa daraja na kuwa Hospitali ya Mkoa mwaka 1963 wakati huo ikihudumia kiasi cha wakazi 336,204.  Kwa sasa  idadi ya wakazi imeongezeka na inakadiriwa kuwa 1,551,766   Ongezeko hilo ni zaidi ya asilimia 462.  Kutokana na ongezeko hilo, Hospitali inahudumia wagonjwa kati ya 300 – 600 kwa siku.  Aidha, ina jumla ya vitanda 275 na inalaza wagonjwa wapatao 136 kwa siku na kuna jumla ya wodi 13.  Mahitaji ya huduma bora yanaongezeka,  wagonjwa wanaongezeka, magonjwa pia yameongezeka, uhitaji wa mafunzo kwa wafanyakazi wa Hospitali wakiwemo Madaktari na  Wauguzi  na wanafunzi kutoka  vyuo  vikuu  mbalimbali hapa nchini pia umeongezeka.  Aidha, hayo yakijumuishwa na ongezeko la maradhi na ajali za barabarani vilisababisha kuzaliwa kwa wazo la kujenga Hospitali itakayoweza kukabiliana na changamoto hizo.