WANANCHI 3242 WANUFAIKA NA HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA KANDA YA KATI.
Posted on: July 9th, 2025
Kambi ya Matibabu ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia Kanda ya Kati imeweza kuwahudumia wananchi 3,242 na kuwapatia huduma katika maeneo tofauti tofauti ya kibingwa.
Hayo yamebainisha na Mwenyekiti wa kambi hiyo Dkt. Amani Malima wakati wa ufungaji rasmi wa kambi hiyo Mei 9, 2025 Mkoani Singida, ambapo amesema zoezi hilo lilianza rasmi Mei 05, 2025 hadi kufikia leo, katika jumla hiyo wananchi 26 wameweza kuhudumia kwa Msamaha.