UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO LA KUFUA HEWA TIBA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA KATIKA MBIO ZA MWENGE 2025.
Posted on: July 21st, 2025
Akipokea taarifa hiyo ya mradi wa jengo la Kufua Hewa Tiba Ndg Ismail Ali Ussi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, amempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuboresha sekta ya Afya kwa kuwekeza katika kuboresha Afya za Wanasingida na Watanzania wote.
Ameendelea kumpongeza Mhe. Dkt. Samia kwa Mradi huu wa Jengo la Kufua Hewa Tiba la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwani litaokoa mambo mengi kama gharama za kufuata hewa tiba hii Mikoa mingine na kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wenye uhitaji wa Hewa tiba hii ya Oksijeni.
Aidha amewapongeza Madaktari, Wauguzi na Watumishi wote wa Sekta ya Afya kwa kazi kubwa wanayoifanya kila siku ya kupambana na magonjwa mbalimbali kama ugonjwa wa VVU/UKIMWI kwani wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasingida na watanzania wote kwa ujumla wanakuwa salama kiafya. “Afya ni mtaji” amesema Ndg. Ismail.