Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AONGEA NA WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA

Posted on: February 21st, 2022

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalage leo Februari 21, 2022 amewasili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida na kuzungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.


Dkt. Seif amewakumbusha watumishi wote wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Pia amewaasa watumishi wote kuepuka tabia ya tamaa na kuhakikisha wanapanga bajeti zao kwa kuzingatia viwango vyao mshahara.