Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MJINI MHESHIMIWA MUSA SIMA ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SINGIDA KWAAJILI YA KUZINDUA NA KUKABIDHI GARI MPYA ILIYOTOLEWA NA SERIKALI.

Posted on: January 3rd, 2024

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mheshimiwa Musa Sima ametembelea vitengo mbali mbali vya kutolea huduma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida. Ametembelea jengo la X Ray na kuona mashine mbalimbali kama vile Digital Xray na CT Scan, ametembelea pia Telemedicine  (Tiba Mtandao) na kuona jinsi inavyofanya kazi na kusaidia katika utoaji wa huduma pia amefika Maabara na kujionea mashine mbalimbali za kutolea huduma za vipimo.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. David Mwasota akimkaribisha muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Bi Yasinta Alute ili na yeye aweze kumkaribisha Mheshimiwa Mbunge amemshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuboresha sana huduma za Afya ikiwa ni pamoja na kuhakisha Hospitali za Rufaa zinakuwa na magari kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Hospitali. Nae Bi Yasinta Alute kwa Niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa akimkaribisha Mbunge wa Jimbo la Singida ameshukuru Ujio wa Mbunge huyo wa jimbo la Singida Mjini pia ameishukuru serikali kwa kutoa gari hilo kwani litasaidia sana katika matumizi mbalimbali ya kutoa huduma hospitalini hapo hususani kwa upande wa watumishi.


Akitoa hotuba fupi kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Singida Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mheshimiwa Musa Sima amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kuwezesha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kupata Mashine  mbalimbali za kutolea huduma sambamba na hilo amepongeza pia huduma ya Tiba Mtandao kwani imesaidia sana kwenye masuala ya rufaa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kwenda Hospitali zingine. Pia amewataka Uongozi na watumishi wote kwa ujumla kutangaza huduma zinazotolewa Hospitalini hapo. Zaidi amepongeza uongozi wa Hospitali na kuwaasa kuendelea kuchapa kazi.

Baada ya kusema hayo Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mheshimiwa Musa Sima alizindua na kukabidhi gari mpya aina ya Toyota Landcruser rasmi kwa ajili ya kuanza kutumika na aliwasisitiza viongozi wa Hospitali kuhakikisha gari hiyo iliyotolewa na serikali inatunzwa vizuri.