Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA APONGEZA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA DHARULA (EMERGENCY) NA WAGONJWA MAHUTUTI (ICU)

Posted on: February 25th, 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa. Abel Makubi leo Februari 26, 2022 amewasili Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa jengo la dharula (Emergency) pamoja na jengo la wagonjwa mahututi (ICU).

Profesa Makubi amesema ujenzi wa jengo la dharula pamoja na jengo la wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida unaendelea vizuri na anaimani ujenzi huo utakamilika katika muda uliopangwa.