Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa Mandewa)

JENGO LA KUFUA HEWA TIBA NA USIMIKAJI MITAMBO SINGIDA RRH LAWEKWA JIWE LA MSINGI LEO JULAI 22, 2025 NA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2025.

Posted on: July 21st, 2025

Akisoma Taarifa hiyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Dkt. David J. Mwasota amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi zake za kuimarisha na kuboresha huduma za Afya ndani ya mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla.

Vile vile Dkt. David J. Mwasota ameeleza ni jinsi gani Mradi huu wa jengo hili la kufua hewa tiba litakavyosaidia kuboresha huduma za Afya zitolewazo Singida RRH na kunufaisha wana Singida. Ameeleza kuwa Mradi huu utahudumia wakazi zaidi ya 2,008,053 wa Mkoa wa Singida na kuwahakikishia kuwepo kwa hewa tiba wakati wote kwa wagonjwa wenye uhitaji.

 

Pia mradi huo utapunguza gharama ya kununua Hewa Tiba nje ya Mkoa ambapo Hospitali imekuwa ikitumia wastani wa kiasiha shilingi 9,000,000.00 kwa mwezi kwaajili ya kununua hewa tiba  Mkoa wa Dodoma na Manyara.