Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Nafikaje Singida RRH

Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Singida inafanya shughuli zake za matibabu katika sehemu mbili ambazo ni;

  1. Hospitali ya mkoa ya zamani iliyopo mjini karibu na ofisi za Posta Singida.
  2. Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa iliyopo eneo la Mandewa, Manispaa ya Singida.

Unaweza kufika sehemu zote mbili kwa kutumia usafiri binafsi, wa umma au wa kukodi.

  • Kwa kutumia usafiri wa umma  sehemu zote mbili zinafahamika vizuri kwa madereva hasa wa BAJAJ na Piki piki (Boda boda) hivyo mueleze dereva uendako nae atakufikisha.
  • Kwa kutumia usafiri binafsi ili kufika Hospitali ya zamani ya mkoa  ukiwa unatokea mjini kati, fuata barabara ya Arusha kuelekea ofisi ya Posta Singida/ uelekeo wa Bomani na baada ya kupita ofisi ya Posta utakua umefika. Na ukiwa umetokea Bomani basi fuata barabara ya Arusha kuelekea mjini kati  na utakapofika chuo cha maabara punguza mwendo kwani chuo hicho ndicho kinapakana na Hospitali ya mkoa ya zamani.

Ili kufika Hospitali mpya ya Rufaa ya mkoa wa Singida kwa usafiri binafsi ukiwa unatokea mjini fuata bara bara ya Mwanza mpaka makutano ya barabara ya  Mwanza na Sepuka kisha fuata barabara  ya Sepuka umbali wa 3.88 Km (2.41 Mi) kutoka makutano hayo ya barabara. Baada ya kwenda umbali huo upande wa kushoto utayaona ukuta wa Hospitali na majengo na utakua umefika.