Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida
(Hospitali ya Mkoa)

Kliniki ya Daktari Bingwa wa magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi.

Posted on: November 12th, 2024

Akina mama wanapata huduma za uzazi pamoja na matibabu ya magonjwa ya wanawake. Aidha tunafurahi kusema kuwa huduma tunazotoa kwa akinamama na wanawake kwa ujumla ni huduma za kibingwa kwani Hospitali ya rufaa ya mkoa tumebahatika kuwa na Daktari Bingwa - Mshauri wa  Magonjwa ya Wanawake na Afya ya Uzazi Mama na Mtoto. Pia unaweza kupata ratiba ya kazi ya idara hii kwenye sehemu ya huduma zetu. Karibu sana tukuhudumie.